Elimu ya Utunzaji wa kumbukumbu wahitajika Wilaya ya Kishapu

Belinda Habibu

Utunzaji wa kumbukumbu husaidia watu pale wanapotaka kuona walikotoka wapi kimahesabu,na kufanya tathimini ya mapungufu ama kujipongeza kwa kufanya vizuri.

Kijijini Idukilo na baadhi ya vijiji vingine vinavyozunguka mgodi mkongwe wa almasi wa Williamson Diamond,wanapata kiasi cha fedha sh. Milioni 156 kwa aajili ya shughuli zao za maendeleo kutoka kwa mwekezaji huyo kwa mwaka.

Mgawanyo wa fadha hizo unapaswa kila kijiji kupata milioni 19.5,lakini wanachokipata kwa kijiji kimoja ni sh. 12,500.

Pamoja na kupata kiasi hicho cha fedha lakini suala la kutunza kumbukumbu limekuwa tatizo kwa kuonyesha kukosa uwelewa miongoni mwa viongozi wa vijiji.

Katika kijiji cha Idukilo wilayani Kishapu, mwenyekiti wake John Kadama alisema kutokana na ofisi yao kutokuwa imara basi mjumbe aliyechaguliwa wa kusaini hela wanazopokea kutoka kwa mwekezaji huyo,huziifadhi risiti za kumbukumbu za mahesabu nyumbani kwake.

Ameongeza kwa sasa sitaweza kuonyesha risiti za mwanzoni tulipopokea hela kwa kuwa aliyekuwa anazihifadhi a lifariki na hatukuzipata tena.

Katika kijiji cha Mwadui Lohumbo serikali ya kijiji imeweza kuhifadhi zilikuwepo ila zimekosewa na kurudiwa rudiwa kwa peni kiasi kwamba kuonyesha kunawalakini katika matumizi ya fedha hizo.

Mwenyekiti wa mzunguko kwa vijiji vyote vinane vinavyozunguka mgodi wa Mwadui, Mbalu Kidiga alisema walishaambiwa na halmashauri kutumia risiti zake na si zinginezo hivyo kama wenyeviti wa vijiji hawajabadilika basi ni kukosa kuchukua hatua za kiutendaji.

Pamoja na ufafanuzi wake pia hata risiti za kijiji cha Maganzo ambazo ni za halmashauri, zinazoonyesha malipo kwa hela zinazotolewa na mwekezaji huyo, zimekosewa na kuonyesha bado hakuna umakini na elimu juu ya utunzaji wa kumbukumbu pindi zitakapohitajika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *