Karibu Utete tuvuke na MV UTETE

Stella Mwaikusa

MV Utete ni kivuko kinachopatikana  katika wilaya ya Rufiji mkoani pwani na kinafanya kazi zake  Mto rufiji, ambapo wakazi wa utete hutumia kivuko hicho kwenda ng’ambo ya pili sehemu zenye mashamba na makazi ya watu.

Kivuko hicho pia kimekuwa kikiwavusha wanafunzi wanaoishi vijiji vya Luwe na Mkongo wanaosoma utete wilayani, na kuwa msaada mkubwa wa kuvusha magari kutoka Ng’ambo ya pili, na kwenda wilayani utete ambako huduma nyingi za kijamii zinapatikana ikiwemo hospitali, ofisi mbalimbali za kiserikali, shule na vyuo.

mv-utete

“ Kivuko kinasaidia sana pale tunapokuwa na mgonjwa kwa sababu kuzunguka na gari la wagonjwa mpaka kituo cha afya cha Kibiti, lakini tukipita hapa ni rahisi kumfikisha mgonjwa hospitali ya wilaya kwa wakati” Anaeleza  Tarcis Bwakila Mganga mkuu wa kituo cha afya cha Nyaminywiri.

Kivuko hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa vijiji vya Luwe, Mkongo,Nyaminywiri na Utete wilayani Rufiji, pia imewarahisishia waendesha pikipiki wa Ikwiriri, ambao hutumia kivuko hicho kuvusha pikipiki zao kwani wanasema njia hiyo ya mkongo kupitia mto rufiji ni njia ya mkato.

Kivuko hicho kina miaka mitatu tangu kianze kufanya kazi zake, na watumiaji wa kivuko hicho wanasema wanamshukuru Mbunge wao wa zamani Dk Mtulya ambaye alisimamia kikamilifu kuhakikisha kivuko hicho kinakuwepo hapo.

Bei za kivuko kwa abiria ni sh 200 huku magari yakivushwa kwa shilingi 500 .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *