Loliondo ya ziwa Nyasa

Albano Midelo

Hapa ni mahali katika kijiji cha Mkili mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma ambapo pamepewa jina la Loliondo, sio kwa sababu kuna mganga ambaye anatoa tiba kama ilivyokuwa kwa babu Loliondo ambako  wengi walikwenda kupata kikombe la hasha.

Eneo hili limepewa jina la Loliondo kwa sababu ndiyo eneo pekee katika kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya 4000 ambako mawasiliano ya simu ya mtandao wa Vodacom pekee yanapatikana.

Hivyo basi kila mmoja anapotaka kuwasiliana anatoka sehemu mbalimbali za kijiji kati ya kilometa  tano hadi  tisa na kufika eneo hilo kuwasiliana kwa kupiga simu au kuandika ujumbe na kusoma ujumbe ambao ametumiwa .

Ukitembelea majira ya jioni kwenye eneo hilo unakuta watu kati ya 30 hadi 50 wakiwasiliana kwa simu na kwamba hakuna siri kwa kuwa utakachokuwa unaongea kwenye simu kila mmoja anakisikia labda uandika ujumbe wa maandishi.

Mitandao mingine yote haipatikani ndani ya kijiji hicho,ni changamoto kwa makampuni ya simu kuwasaidia wananchi hao ili waweze kuwasiliana kwa urahisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *