Marupurupu yatangazwa watakao ajiriwa sekta ya afya Ileje

Gordon Kalulunga

WAKATI watumishi wengi wakiwa wanakimbia wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kutokana na kinachodaiwa kuwa ugumu wa mazingira. Watumishi watakao ajiriwa katika sekta ya afya wilayani humo, watanufaika na motisha itakayotolewa na halmashauri hiyo kwa lengo la kuwavutia ili wasikimbie kufanya kazi katika wilaya hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Mganga mkuu wa wilaya ya Ileje Christopher Jakoracha alisema kuwa kutokana na upungufu wa watumishi katika sekta ya Afya ambao unatokana na watumishi wengi kuikimbia wilaya hiyo halmashauri imejipanga kuwapa motisha watumishi watakaokubali kufanya kazi wilayani humo.

Jakoracha alisema kuwa baadhi ya mambo ambayo halmashauri imekusudia kuyafanya kwa watumishi hao ni pamoja na kuwalipa posho zao pindi wanapofika kwa ajili ya kufanya kazi, kitanda cha kulalia pamoja na godolo la kuanzia na chakula kwa siku atakazokuwa akisubiri mshahara wake wa kwanza.

Aliongeza kuwa vitu vingine vitakavyotolewa ni pamoja na piki piki kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa mtumishi atakayepelekwa katika maeneo yenye miondombinu mibovu ili aweze kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi zaidi.

Mganga mkuu huyo alisema hadi hivi sasa tayari piki piki (5) ziko tayari na zimefika Halmashauri na nyingine (7) ziko kwenye bajeti ambayo inaishia mwezi wa sita hivyo aliongeza kuwa iwapo yote hayo yatatimizwa na ni dhahili kuwa watumishi katika halmashauri hiyo hawatoweza kuikimbia tena kama ilivyo hivi sasa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sylvia Siriwa alisema kuwa changamoto inayoikumba Halmashauri hiyo ni watumishi kuikimbia katika kufanya kazi jambo ambalo alisema wameliona na wanataka kulitatua kwa kutoa vivutio kwa watumishi.

Siriwa alisema kuna mikakati mingi ambayo baadhi yake hawezi kuiweka wazi kwa sasa ila muda ikifika ataiweka wazi ili jamii itambue na watumishi watakaletwa katika halmashauri hiyo wajue nini watanufaika wakiw wilayani humo.

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha watumishi katika sekta mbali mbali za halmashauri hii wasikimbie kufanya kazi na tutahakikisha kuwa mipango yetu inakwenda kama tulivyo panga ili watumishi waongezeke” alisema Siriwa na kuongeza.

“Katika halmashauri hii tunaupungufu wa watumishi kwenye sekta ya afya kwa asilimia 48 wakati kwenye sekta nyingine inahitajika watumishi kwa asilimia 52 ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo”

Hadi sasa kuna Zahanati 5 ambazo hazina watumishi kabisa na hazijafunguliwa kutokana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na dawa lakini vile vile kuna zahanati zaidi ya 5 ambazo nazo zitakamilika muda sio mrefu hivyo watumishi wanahitajika sana.

4 Comments
  • Nimevutiwa na tangazo lenu natamani kufanya kazi katika ofisi yenu nimemaliza chuo cha utumishi wa umma kozi ya utunzaji wa kukumbu ngazi ya cheti

  • Nimevutiwa na tangazo lenu natamani kufanya kazi katika ofisi yenu nimemaliza chuo cha utumishi wa umma kozi ya utunzaji wa kumbukumbu ngazi ya cheti

  • mbona kuna watumishi wa afya wapo nyumbani hawana ajira. tatizo ni serikali yenu haina hela za kuajiri wahudumu wa afya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *