Mashirika ya Tanzania yatuhumiwa kukithiri kwa uhalifu wa kiuchumi duniani

Jamii Africa

Daniel Samson

Licha ya kuimarika kwa mapambano dhidi ya rushwa nchini, Tanzania bado iko kwenye kiwango cha juu cha uhalifu wa kiuchumi na udanganyifu mali unaotokea kwenye mashirika ya umma na binafsi

Uhalifu wa kiuchumi na udanganyifu katika mashirika unahusisha  vitendo vya kujipatia fedha kwa njia isiyo halali ambao ni matokeo ya kuchezewa kwa mifumo ya fedha ya mashirika ambako kunatoa nafasi kwa mtu au kikubdi cha watu  kutumia vibaya fedha zilizoidhinishwa kwa matumizi halali.

Kwa mujibu wa shirika la PwC Global  lilitoa matokeo ya utafiti kuhusu Uhalifu wa kiuchumi na Udanganyifu (2017) limebaini kuwa uhalifu wa kiuchumi nchini Tanzania umefikia asilimia 57 ambapo ni kiwango cha juu ukilinganisha na wastani wa dunia ambao ni asilimia 49.

 NCHI 10 ZILIZORIPOTIWA KUWA KIWANGO KIKUBWA CHA UHALIFU WA KIUCHUMI 

                            Chanzo: Global Economic and Fraud Survey

Aina ya uhalifu unaojitokeza Tanzania ni ishara kuwa rushwa imeathiri ukuaji  wa uchumi na heshima ya nchi katika mipaka ya kimataifa. Ripoti ya utafiti huo inaonyesha kuwa Matumizi mabaya ya mali za umma yamejitokeza zaidi yakifuatiwa na udangajifu wa watumiaji wa huduma za kijamii na idara za manunuzi.

“Hii inaonesha kuwa mfumo mzima wa manunuzi umetawaliwa na uhalifu”, inaeleza ripoti hiyo.

Sakata la mkataba tata kati ya kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi ambao ulisababisha kupotea kwa bilioni 34 kati ya bilioni 39 ambazo zilitolewa kwa kampuni  hiyo kutekeleza mradi wa kufunga mfumo wa utambuzi wa alama za vidole katika vituo vya Polisi 138 nchini tangu mwaka 2011.

Kulingana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilionyesha kuwa mradi huo haukutekelezwa kikamilifu licha ya mzabuni huyo kupewa asilimia 99 ya fedha yote ambapo walifunga mfumo huo katika vituo 14 tu nchi nzima.

Kashfa hiyo iliwaibua Kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulikia Hesabu za Serikali (PAC) ambapo mwaka 2017 walithibitisha mkataba huo wa manunuzi haukufuata taratibu za kisheria. Kutokana na kashafa hiyo viongozi waandamizi serikalini walijiuzuru.

Utafiti huo uliwahoji wa watu 7,200 kutoka katika nchi 123 duniani ambapo kwa mwaka wa 6 mfufululizo vitendo vya uhalifu wa kiuchumi vimeongezeka na kufikia asilimia 36. Ongezeko hilo linatokana na PwC kuibua matukio mbalimbali yanayotokea duniani.

Afrika inatajwa katika ripoti hiyo kuwa imekithiri zaidi kwa vitendo hivyo ambapo karibu nusu ya matukio hayo yanatokea katika bara hilo. Afrika Kusini na Kenya ndio zinaongoza duniani kwa uhalifu wa kiuchumi.

 

Uhalifu wa kiuchumi na udangajifu wa fedha unaweza kupungua…

PWC imebaini kuwa asilimia 49 ya mashirika duniani yamewahi kukumbwa na uhalifu wa kiuchumi kwa miaka miwili iliyopita. Lakini vipi kuhusu 51% iliyobaki? Wamefanikiwa kujizuia na uhalifu huo au hawafahamu kuwa unatokea?

 

Ni aina gani ya uhalifu wa kiuchumi na udanganyifu  wa fedha unaojitokeza zaidi?

 

 

Nani Anatekeleza udanganyifu wa fedha kwenye mashirika ya umma?

Inaelezwa kuwa asilimia 52 ya matukio hayo hutekelezwa na wafanyakazi wa mashirika (internal actors). Asilimia 68 ni watu toka nje ya shirika ambao huchangia asilimia 40 ya udanganyifu ambapo ni watu wenye mahusiano ya karibu na shirika husika hujumuisha mawakala, wateja, wachuuzi na wanahisa.

Kwa matukio ya udangajifu yanayofanywa ndani ya shirika huratibiwa zaidi na uongozi wa juu ambapo yameongezeka kutoka 16% hadi 24% mwaka 2017. Na 91% ya udanganyifu mkubwa ulijulikana kwa bodi za mashirika lakini hatua stahiki hazikuchuliwa kukomesha uhalifu huo.

 

MAMBO 3 YANAYOWEZA KUTOKEA IKIWA UHALIFU WA KIUCHUMI HAUTADHIBITIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa PwC anaeleza kuwa hasara kubwa imebainika kupatikana kwenye uhalifu wa kiuchumi ambapo theluthi mbili (64%) ya wahojiwa wote walisema hasara waliyoipata kutokana na udangajifu wa fedha ulifikia Dola za Marekani milioni 1. Asilimia 16 walisema ni kati ya Dola milioni 1 na milioni 50.

Hata hivyo, uhalifu wa kiuchumi katika shirika unaweza kudhibitiwa ikiwa utabaini udanganyifu kama umegundua kuna mahesabu yasiyo sawa, kuchukua hatua stahiki pamoja na kuanzisha uchunguzi. Pia kutumia teknolojia ya kisasa katika utendaji wa shirika na mwisho ni  kuwekeza maarifa na ujuzi kwa wafanyakazi kuliko mashine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *