MRADI WA VIPEPEO UTAKAVYOWANUFAISHA WAKAZI WA SAME-KILIMANJARO.

Belinda Habibu

Wananchi wa wilaya ya Same wanaweza wakajikwamua na wimbi la umaskini kwa kujishughulisha na mradi wa vipepeo na kuviuza ndani na nje ya nchi.
Vipepeo wa kila aina wanapatikana kati msitu wa hifadhi wa Shengena uliopo Chome wilayani humo.
Msimamizi mkuu wa msitu wa Shengena Frank Mahenge alisema kwanza wanafanya uhamasishaji kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka msitu huo, kuanza kufuga vipepeo ambao wanasoko hasa nje ya nchi.
Amesema ukifanya biashara ya vipepeo haina hasara kwa kuwa unasafirisha mabuu ambao wanaangulia huko wakifika na hata jinsi ya kuwasafirisha ni rahisi.
Nawasihi wakazi wa wilaya hii kujiajiri wenyewe kwa kuuza vipepeo,kwa kuwa soko lake lipo na gharama ya kuwahudumia vipepeo hadi mabuu yajiweke tayari kwa kusafirishwa ni ndogo.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *