Picha hizi zinaonesha baadhi ya abiria wakijitahidi kumtoa dereva wa basi la Abood aliyebanwa miguu katika ajali.
Basi hilo linasafiri kati ya Dar es salaam na Tunduma Mbeya na lilipata ajali tarehe 3 Oktoba 2011, katika maeneo ya Mafinga mkoani Iringa baada ya kuligonga kwa nyuma basi la kampuni ya Ottawa Express linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Songea mkoani Ruvuma. Katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa
poleni sana kwa ajali
poleni kwa ajali
Jamani haya mabasi ya Abood yazuiwe kusafirisha abiria ,maana kila siku ajali
majeruhi poleni sana
majeruhi wote poleni…