Songea: Mpunga watumika kutengenezea pombe!

Mariam Mkumbaru

Ubovu wa Barabara katika kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi  Wilaya ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma, unasababisha mpunga kutengeneza pombe ya kienyeji.

Pombe hiyo ijulikana kama pombe ya mpunga, inachangwanya kwa mapumba laini ya mpunga,  kwa kuyaloweka kwa siku tatu, pia wanachanganya na uji wa ulezi uliolowe kwa kwa siku tatu.

mpunga-pombeDoris akiuandaa mpunga uliotoka shambani kwa ajili ya kutengenezea pombe ya kienyeji

Baada ya kuchanganya inalowekwa kwa siku mbili, siku ya tatu wanaweka unga wa mchele na kuipika katika pipa kubwa kwa saa tatu, inakuwa imewiva tayali kwa kunywa.

Lita moja Tsh. 400, ubovu wa barabara na kukosa soko la zao la mchele tunaolima kwa wingi ndio unasababisha mchele huo tutengeneze pombe ya mpunga kwa kujipatia kipato.

pombe ya mpungaPombe inatokana na mpunga ikiandaliwa kwa kuchemshwa

“Mazao mengi tunalima lakini hakuna barabara ya uhakika kusafirisha mazao mpaka soko kuu la mazao SODECO Songea, unaweka mpunga ndani mpaka unaliwa na wadudu na kuharibiki, ukiwa na mpunga inakubidi utengeneze pombe ya mpunga ili usiharibike,” Alisema Emanuel Komba.

Wanakijiji wa Ifinga wanalima mazao ya chakula na biashara lakini wanakwama kufikisha katika soko la mazao SODECO kwa ubovu wa barabara, mazao hayo kama mtama, ufuta, tangawizi, ndizi, ulezi, uwele, mpunga, maharage na  miwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Beatrice Msomisi, alikili kuwepo kwa ubovu wa barabara katika kijiji hicho, alisema sio Ifinga tu Vijiji vingi vya Wilaya ya Songea barabara zake ni bovu sana.

Kipindi cha Masika barabara mbalimbali za vijijini hazipitiki kiurahisi kwa sababu ya ubove, sio mazo tuu kuletwa sokoni, hata mgonjwa na kufikisha madawa kwenye Zahanati mbalimbali ni tatizo kubwa.

“Bajeti ninayopewa katika barabara ni ndogo sana napewa Tsh. Milioni 600 kwa mwaka, za kukarabati barabara mbalimbali za vijijini na mjini, pesa ni ndogo sana ukilinganisha na hali halisi ya ubovu wa barabara hizo na ukubwa wake,” alisema Msomisi.

Milioni 600 tunayopewa  kwa ajili ya kukarabati barabara ni ndogo sana ukilinganisha na ubovu wa barabara zenyewe, pesa hiyo ukikarabati barabara kwa kiwango kizuri ikiwa inapitika kipindi cha masika na jua kali unakarabati barabara moja tu. Umbali wakutoka kijijini kwa kutumia gari ni saa 2 na nusu kwa pikipiki ni saa 3 hadi 4.

Aidha aliiomba Wizara husika kuwaongezea pesa katika ukarabati wa barabara  mbalimbali   za  Wilaya hiyo, kwa sababu ziko katika hali mbaya sana na kipindi kama cha masika hazipitiki kabisa na kunakuwa hakuna mawasiliano kati ya Vijiji na Wilaya.

Kutoka Ifinga mpaka kufika makao makuu ya Wilaya ya Songea ni kilometa 219, na kilometa 48 ni barabara ya vumbi, Wilaya ya Songea inaukubwa wa kilometa za mraba 16,000 idadi ya watu kwa sensa ya mwaka huu ni 170,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *