Ukosefu wa Mikataba ya ajira kwa Wachimbaji Wafanyakazi Mererani na changamoto zake

Belinda Habibu

Wafanyakazi wachimbaji wa migodini Mererani  (wanaapolo) wanakabiliwa na matatizo mbalimbali likiwemo la ukosefu wa mikataba ya ajira kutoka kwa waajiri wao.

Wakizungumza na mwandishiwa habari hii katika migodi ya Mererani wachimbaji hao wanasema ukiomba kazi unakubaliwa bila maandishi walakusaini popote.

Mmojawawachimbajihao bwana Hashimu Said Nyambi alisema kutoka na hakuna mikataba kati yao na waajiri wao,wanakosa haki zingine ikiwemo kukosa mshahara,hela ya matibabu,malazi na hata ya chakula.

“Tunakula maramoja kwa siku na chakula hakitoshelezi,kama utakula leo saa tisa basi mpaka kesho saa tisa na tunafanya kazi ngumu”alisema bwana Nyambi.

Ameongeza hakuna mapatano yakugawana kile kinachopatikana,na tunashindwa hata kwenda kusalimia familia zetu tunajikuta tunakaa hapa kwa miaka zaidi ya kumi na tano tukihofia tutaendaje majumbani mwetu wakati hatuna chochote.

Alisema mwaka 1994 hapa Mererani kulikuwa na chama cha kupigania haki za wachimbaji migodini, cha kushangaza kiongozi wetu aliondoka katika mazingira ya kutatanisha na hatimaye chama kile kikafa.

“Kutokana nakukosa mikataba tunaweza kufukuzwa kazi muda wowote,haijalishi umechimba kwa miaka mingapi,na umeathirika kiafya kwa kiasi gani” anaongeza bwanaNyambi.

Mchimbaji mwingine bwana Elipokea Elisante alisema riziki yetu tunaipata kwa kusubiri baruti ikilipuliwa tunaokota vipande vya madini na tusionekane na msimamizi wa mgodi aliyewekwa na mchimbaji mmiliki wa kitalu.

Ameongeza hali hiyo inatokana na kukosa mkataba wa ajira kati ya mchimbaji mfanyakazi na mchimbaji mmiliki wa mgodi,kwani tungekuwa huru kuwa mali hii ina mgawanyo sahihi.

Bwana Elisante aliongeza pamoja na hali hiyo yote,siwezi kurudi nyumbani kwa kuwa kwa miaka tisa niliyokuwepo hapa sijapata chochote na nimeshapoteza muda na kwa elimu yangu ya darasa la saba sijui nitafanyanini,nabakia hapa kupambana.

Mchimbaji mfanyakazi bwana Apollo Olomi alisema kwa kuwa hawana mikataba ya kazi,na upatikanaji wa tanzanite huchukua muda mrefu mpaka mmiliki wa kitalu (mchimbajimdogo) wakati mwingine kushindwa kuendesha mgodi  na kuondoka,tunakuwa katika hali ngumu sana.

“Akiondoka mchimbaji mmiliki wa kitalu,anakuja mwingine anachagua wachimbaji wafanyakazi wengine na haijalishi tumefanya kazi hapo kwa miaka mingapi na tunakosa haki zetu zote”anaalamika bwana Ollomi.

Alisema naiomba serikali kikitokea kitu cha namna hii,wauze mgodi kwa mtu mwingine na tuliochimba muda mrefu (wafanyakaziwachimbaji) tulipwe kiinua mgongo chetu.

Mchimbaji mfanyakazi mwingine bwana John Eliudi kutoka kitalu B  alisema serikali ingefuatilia suala la mikataba kwetu,kwa kuwa wengi tunachimba bila faida yoyote na tunaishi kwa matumaini kuwa ipo siku tutapata tu katika mazingira haya.

“Wachimbaji wengi wametumika bure,wamepoteza muda wao,nguvu na hata maisha yao na wengine kuathirika kiafya bila ya kupata faida  yoyote ile” alisema bwanaEliudi.

Alisema hatuna hata vitambulisho vya kazi ambavyo vitatuwezesha hata tukifukuzwa kuweza kudai haki zetu,nani atakusikiliza wakati haufahamiki?.

Mmiliki wa kitalu D, bibi Stella Shayo alisema ni ngumu kumpa mkataba mchimbaji (mwanaapolo) huwa wanaondoka kutegemeana na utokaji wa madini.

“Wafanyakazi wachimbaji hawana msimamo unaweza ukawanao 30 leo ama 20 wakati uzalishaji bado na wakazidi hadi kufikia miamoja wakati wanapoona madini yanapatikana”anasisitiza bibi Shayo.

Ameongeza kuwa kunakipindi serikali ilituagiza tutengeneze vitambulisho,tulitii agizo hilo,hata hivyo waliahama pamoja na kuwanavyo.

“Meneja,msimamizi wa mgodi,mtaalamu wa miamba,hawa wanamikataba na hawawezi kukimbia lakini wachimbaji wafanyakazi hata wakiwa na mikataba watakimbia tu”.alisema bibi Shayo.

Mkurugenziwa TANSORT (kitengo kinachojishughulisha na kuthaminisha  madini ya vito) wizara ya nishati na madini, bwana Archard Kalugendo, kuhusu suala la ajira kwa wachimbaji wafanyakazi,alisema ni vyema wamiliki wote wa migodi wenye leseni wanapaswa kuangalia sheria zingine zinasema nini,kama sheria ya ajira.

Sheria ya ajira na mahusiano mahali pa kazi (SAMK) ya 2004,inatoa fursa, kusisitiza na kulinda suala zima la uhuru wa wafanyakazi nawaajiri katika kuunda na kujiunga na chama au shirikisho lolote katika maeneo yao ya kazi. Lengo kuu la kujiunga huko ni kulinda na kutetea maslahi yao yaliyo halali kwa mujibu wa Sheria.

Sera ya madini ya mwaka 2009,katika moja ya madhumuniyake, inasema serikali itawawezesha na kuwahamasisha wachimbaji wadogo katika migodi shughuli za uchimbaji ili waweze kuchangia uchumi wataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *