Zifahamu sababu na tiba ya muwasho Sehemu za siri

Jamii Africa

Kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani kujumuisha maradhi ya uke kwa wanawake au muwasho na kuvimba kwa sehemu za siri za wanaume (jock itch). Bila kujali jinsia muwasho unaweza kusababishwa na ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya zinaa au mzio (allery).

Kuwashwa makalioni hutokea pale ngozi inayozunguka njia ya haja kubwa inapokereketa ikiambatana na hamu ya kutaka kupakuna. Muwasho huongezeka pale unapokaa na kukiwa na unyevunyevu. Sababu kuu za kuwashwa matakoni ni kutojisafisha vizuri, kula vyakula vyenye viungo vingi sana, kuhara, vidonda kwenye njia ya haja kubwa, maambukizi ya fangasi, bawasiri(hemorrhoids), minyoo na kadhalika.

Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe kitu hicho kikiondolewa. Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi, ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.

Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanaume?

Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu zingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa, mzio, maambukizi ya bakteria n.k

Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanamke?

(1) Maambukizi ya Fangasi Ukeni (Vaginal Yeast Infection)
Ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni uwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

(2) Ugonjwa wa kuvimba uke (Vulvovaginitis)
Ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.

(3) Kuvimba Uke baada ya hedhi kukoma (Postmenopausal Atrophic Vaginitis)
Ni ugonjwa wa kuvimba kwa uke baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

(4) Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomonas Infection)
Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu ni muwasho katika uke au uume na kutokwa na uchafu ukeni.

(5) Ugonjwa wa Minyoo (Pinworm Infection)
Ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea sana watoto wa kati ya miaka 5 na 10.

(6) Inflamesheni ya Urethra (Urethritis)
Ni maambukizi kwenye urethra (ujia wa kutolea mkojo nje) yanasababisha kuvimba kwa urethra. Dalili kuu ni mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa uchafu.

(7) Genital Warts
Ni vivimbe vidogo vinavyotokea juu ya ngozi sehemu za siri. Ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiana na unasababishwa na virusi viitavyo Human papillomavirus (HPV). Vivimbe vinaweza sababisha muwasho na maumivu.

(8) Saratani ya sehemu ya nje ya Uke (Vulvar Cancer)
Ni saratani ya sehemu ya nje ya uke inayoambatana na kuwashwa sehemu ya nje ya uke.

(9) Ugonjwa wa Wasiwasi (Generalized Anxiety Disorder)
Ni ugonjwa ambao unaotokana na hofu ya matukio fulani. Wakati mwingine husababisha kujikuna sehemu mbalimbali hata sehemu za siri.

(10) Ugonjwa wa Sjogren (Sjogren's Syndrome)
Ni ugonjwa katika mfumo wa kinga ya mwili unaoathiri tezi zinazosaidia mwili kutengeneza unyevu nyevu kwenye macho na mdomo. Ugonjwa huu huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.

(11) Kisukari
Ni ugonjwa sugu wa kimetaboliki unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa Insulin au utendaji kazi wake. Kisukari kilichokomaa kinaweza sababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.

Wanaume wanapaswa kufuata hatua zifuatazo ili kusaidia kuepuka kuwashwa sehemu za siri :-
– Kuosha vizuri uume, na kwa wale ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani za govi.
– Ziweke sehemu zako za siri kutia ndani makalio katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana unyevunyevu unaweza sababisha maambukizi. Matumizi ya poda ya Cornstarch yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali.
– Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani (chupi) angalau kila siku.
– Vaa kondomu kila unapofanya ngono na mwanamke usiyejua hali yake kiafya kiujumla.

Wanawake wanapaswa kufuata hatua zifuatazo ili kusaidia kuepuka kuwashwa sehemu za siri:-
– Baada ya kukojoa au kujisaidia, osha sehemu zako za siri kuanzia mbele(ukeni) kwenda nyuma(matakoni) ili kuzuia bakteria kutoka njia ya haja kubwani kuingia ukeni.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *