Mwandishi aliyekataa kuibeba CCM atimuliwa Igunga

Jamii Africa

Mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Arodia Peter, ambaye amesafirishwa na kulipiwa na CCM Igunga, ametimuliwa na kutishwa na vijana wa ulinzi wa CCM katika mkutano wa chama hicho uliokua unahutubiwa na Waziri wa Miundombinu Dr. John Magufuli mjini Igunga, tofauti na ule wa Mkapa vijijini. Mbali ya kumtimua mwandishi huyo vijana hao wamemtishia na taarifa kutolewa polisi ambapo ilifunguliwa jarada lenye namba RB GURB/1731/2011, Kimsingi wamesema wakimuona watamvunja.
Hiyo si mara ya kwanza kwa mwandishi huyo kupata kibano toka CCM na mwanzo ikiwa ni kuzuiwa kuingia wala kusogea ktk hoteli walipo CCM ya Peak. Inaelezwa sababu kubwa ya mwandishi huyo kupewa kibano na CCM ni habari zake za msimamo ikiwamo kukamatwa ka viongozi wa CCM kwa kuvamia na kushusha bendera ya Chadema kabla ya kutaka kupigwa na wananchi.
Habari ingine iliyowakera ni ile ya kusema ahadi za Magufuli katika uchaguzi ni za kisanii ikiwamo ile ya Busanda. Na habari ya tatu ni ile iliyoelezea CCM kuteka wana chadema watatu. Matukio yote hayo yalikemewa na viongozi wa CCM na polisi akiwamo Kamanda Mungulu na watu wa kitengo cha habari wa CCM, Daniel Chongolo na Gabriel Athumani na CEO wa New Habari, Hussein Bashe.

2 Comments
  • CCM utawala umefikia ukingoni maana mafisadi wataimaliza! Marehemu Kolimba alishahitimisha msumali wa kifo chake! CCM kukosa dira na mwelekeo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *